KWANINI BAADHI YA WATU HUPATWA NA HAYA??

Je wazo la kujumuika na watu katika sherehe au kuzungumza mbele yao linakufanya ujiulize nitasema nini?

Kama jibu lako ni ndio, basi haupo peke yako.

Akindele Michael alikuwa mtoto mwenye haya sana.

Alikulia Nigeria na muda wake mwingi kujifungia ndani ya nyumba kwa sababu hakutaka kutangamana na watoto wengine.

Lakini wazazi wake walikuwa tofauti kabisa na yeye. Anaamini amekumbwa na haya kutokana na jinsi alivyolelewa.

Kuna ukweli wowote kuhusiana na dhana hii?

Kwa kiwango fulani, anasema Thalia Eley, Profesa wa masuala yanayohusiana na tabia inayotokana na kukua kwa mfumo wa jeni, katika chuo cha Kings College London.

70% ya tabia ya kuona haya hutokana na mazingira mtu amekulia

"Tunafikiria haya hutokana na maumbile ambayo ni chanzo cha kuelezea tabia ya mtu," anasema.

"Watoto wadogo wanapoanza kutangamana na watu wengine kando na wazazi wao utaona tofauti na maranyingi hawafurahii kwasababu hawajawazoea."

Anasema ya kuwa ni karibu 30% tabia ya haya ambayo husababishwa na mfumo wa jeni lakini mambo mengine yote huchangiwa na mazingira ya mtu.

Baadhi ya mambo tunayojua kuhusiana na mfumo wa jeni unaomfanya mtu kuwa na haya yameangaziwa katika utafiti ambao unalinganisha haya kati ya mapacha wanaofanana na ambao mfumo wao jeni ni moja.

Katika enzi za hivi karibuni wanasayansi kama Eley, wameanza kuchunguza chembe chembe ya vinasaba, DNA ili kubaini ikiwa mabadiliko yake yanaweza kuathiri tabia ya mtu au afya yake ya akili.

Kila mtu ana tofauti ndogo ya kimaumbile ambayo huathiri kwa kiwango kidogo sana tabia ya mtu lakini kiwango hicho kikiwa juu utamuana muathiriwa akipendelea sana kujitenga na watu mengine huchangiwa na mazingira ambayo mtu amekulia.

Kwa hivyo mazingira ni muhimu katika ukuzaji wa tabia ya mtu.

Kwa mfano mtoto mwenye haya huenda akajitenga na wenzake hata wakiwa wanacheza pamoja, hashiriki vilivyo katika mchezo huo bali anaangalia wenzake wanafanya nini.

Hali hiyo inawafanya wajisikie huru zaidi kwasababu hivyo ndivyo walivyo na mwisho huwa mezoea.

"Suala muhimu hapa sio kuwa ni kigezo kimoja ama kingine; ni vyotr [mfumo jeni na mazingira hufanya kazi pamoja," anasema Eley.

"Ni mfumo imara. Kwa sababu ya hilo, unaweza kubadilisha hali hiyo kupitia tiba ambayo itakufunza jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo."

Mtoto mpole huenda akajitenga na wenzake kwasababu anafurahia kuwa mwenyewe

Ni ajabu mtu kuona haya?

Chloe Foster, Mwanasaikolojia katika kituo cha kushughulikia matatizo ya msongo wa mawazo na wasiwasi wa kupitiliza mjini London amesema kuwa na haya ni jambo la kawaida na haisababishi matatizo hadi pale inapokuwa mtu anakuwa na matatizo ya kutangamana na wengine katika jamii au kushikwa na kiwewe cha kupitiliza.

Foster anasema anaowatibu hutafuta msaada kwasababu wanaanza kuepuka mambo mengi ambayo wanapaswa kuyafanya.

Mathalani kutoweza kuwasemesha watu kazini, kupata ugumu kujumuika na watu au kuwa katika hali ya kuhisi kuwa wanahukumiwa au kupimwa na watu wengine.

Matibabu ya kushughulikia matatizo ya kisaikolojia na kijamii yanayojulikana kama Cognitive Behavorial Therapy (CBT) ni miongoni mwa mifumo ya matibabu inayowasaidia pakubwa watu walio na matatizo ya kiwewe na haya ya kupitiliza.

Eley anasema huenda kuna sababu za kwanini watu wanaanza kuwa na tabia za kuwa na haya.

'' Ni muhimu kwa mfano kuwa na watu katika kundi lako ambao hujitokeza zaidi, wanadadisi mambo na kutangamana na makundi mapya lakini pia ni muhimu kwa watu ambao hawataki kuthubutu, wanazingatia pakubwa hatari na athari na walio na weledi mkubwa zaidi katika kuwalinda watu wenye umri mdogo''

Mwanasaikolojia huyo anasema tiba ya CBT ndiyo bora zaidi kwa ajili ya watu wanaoshindwa kutanagamana kwa urahisi na wengine au walio na kiwewe na tiba hii inafanya kazi kwa kujaribu kubadilisha mawazo yako na mfumo wa tabia zako.

Angazia hadhara unayohutubia kuliko kujiangazia wewe binafsi ili usijipate unatafuta maneno ya kusema au kusahau kile unachotaka kusema., wataalamu wanasema

CBT inakusaidia kutambau mawazo hasi pamoja na kutambua tabia fulani ambazo tunadhani zinaweza kutusaidia kukabiliana na haya au kiwewe kama kukariri kile tutakisema kabla au kuepuka kuangiliana na mtu machoni.

Foster anasema mara nyingi ni picha ya mtu anayetunyanyasa huja akilini kabla, wakati na baada ya tukio la kijamii. Wakati mwingine tatizo ni watu walio na matatizo ya kuzungumza hadharani kutokana na haya mara nyingi hujiwekea vigezo vya juu mno kuhusu wanapaswa kujiendesha vipi.

"Huenda wakafiri hawapaswi kutetereka wanapozungumza au wanapaswa kuonekana wachangamfu mno na kila mtu anapaswa kuguswa au kuvutiwa wakati wote na kile anachokisema."

Jinsi unavyojihusisha katika hafla na masuala ya kijamii ndivyo unavyojenga uwezo wakeo wa kujiamni anasema Chloe Foster akiongeza iwapo watu walio na haya au kiwewe wanaweza kujiondolea wenyewe sehemu ya shinikizo kubwa la kukubalika au kutambulika katika jamii, wakijipa nafasi ya kuvuta pumzi na kuwa na vituo huenda ikawasaidia kupunguza kiwewe.

Kitu kingine ambacho kinaweza kukusaidia ni kujaribu kuangazia kwa makini kile kitu kinachofanyika mbele yako badala ya kuangazia kile unachowaza akilini wakati huo.

Angazia hadhara unayohutubia kuliko kujiangazia wewe binafsi ili usijipate unatafuta maneno ya kusema au kusahau kile unachotaka kusema.

Mtindo wa maisha wa watu ughaibuni unasisitiza umwangalie mtu machoni ukisema naye- lakini si kila tamaduni inakubali hili.

Pia anapendekeza ujaribu kufanya kila uwezalo kufanya mambo ambayo hujazoea ili upate ujasiri.

"Hakuna mtu alizaliwa akiwa na uwezo wa kufanya kila kitu. Kila unapofanya jambo geni ndivyo unapata ujasiri wa kujiimarisha," anasema.

"Lakini kumbuka kutumia mbinu tofauti ambazo utakuwa huru wakati unajarribu kufanya kitu kipya kama kuzungumza mbele ya hadhara."

Hii inamaanisha kubadilisha mawazo yetu kabisa. Hebu jiulize ni kitu gani unachoogopa sana ukiambiwa uhutubie kundi la watu. Je unaogopa watu hawatavutiwa na hotuba yako ama unaogopa utaishiwa na kitu cha kusema? Kadri unavyoweza kung'amua ni mabo gani yanakupatia changamoto ndivyo utakavyopata ujasiri wa kukabiliana na changamoto hizo.

Jessie Sun, mwanafunzi wa PhD katika chuo kikuu cha California Davis ambaye pia ni mtafiti wa saikolojia ya binadamu,anasisitiza kuona haya na upole ni vitu viwili tofauti.

Post a Comment

0 Comments