JE, UNAFAHAMU FAIDA 5 ZA KULA TANGO??

Tango ni tunda mojawapo lenye maji mengi kama vile tikiti maji, linabeba virutubisho vingi vitamin K, B, C, Potasium, na manganese.

Tango lina polyphenols ambayo inasaidia kuepusha mtu kupata maradhi sugu, hivyo ni vizuri mtu kutumia matango mara kwa mara kwa kunywa juice yake, kuchanganya kwenye kachumbali bila kumenya maganda yake kwani yanabeba virutubisho vizuri au unaweza kuweka kwenye mkate na kuchanganya na maji ya kunywa kuyapa ladha na Vitamins.

Zipo faida nyingi mwilini za kutumia tunda la tango, ikiwa ni pamoja na.

Kutoa harufu mbaya mdomoni

Inashauriwa kutumia kipande cha tango kuweka mdomoni kwa dakika 5 kwa angalau mara 3 kwa siku inasaidia kutoa bakteria wanaofanya mdomo kutoa harufu mbaya.

2. Husaidia kupunguza uzito na mmeng’enyo uende vizuri.

Kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kusaidia upunguze uzito kamba kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmengenyo wa chakula.

3. Husaidia wagonjwa wa kisukari

Hupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu la aina zote mbili ”Low and High blood pressure” pia tango lina homoni ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho ili kuwezeza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo huwasaidia wagonjwa wa kisukari.

4. Husaidia afya ya viungo, huondoa ugonjwa wa baridi yabisi.

Tango bi chanzo cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo, pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C na D, Folate, Calcium, Magnesium na Potasium ambapo linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu magonjwa ya Gout na yabisi kwa kupunguza kiwango cha tindikali.

5. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

6. Tango husaidia kupunguza aina mbalimbali za kansa.

Kama vile kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa mwanamke, kansa ya kizazi kwa wanawake, na kansa ya tezi dume kwa wanaume hii ni kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika tango kama vile, Iariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol.

7. Tango pia huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani ina vitamin B ambazo husaidia kuounguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila inatakiwa kula kabla ya kulala ili umake ukiwa vizuri.

Post a Comment

0 Comments