HII INAWAHUSU WADADA TU, SOMA HII

Inaelezwa, wakati watu wote wakimfurahia na kumpenda Daudi Huko Yerusalemu, mke wake Mikali alikuwa akimdharau na akiyachukulia poa mafanikio yake.
.
Wakati wanawake wote huko Persia wakiwa na hamu ya kuingia katika Kasri ya Mfalme Ahasuero, walau waguse pindo la vazi lake, Mkewe Mfalme, Malikia Vashti alionesha kiburi kwa mfalme.
.
Point yangu iko wapi?
.
Sio wanaume pekee ambao hawafahamu kuwa wanao wanawake ambao ni wife material, bali, hata wanawake wengi hawajui kama wako na wanaume bora.
.
Hili ni kosa kubwa sana la kiufundi ambalo wengi hulifanya. Katika kipindi cha usichana wao, huwakimbia wanaume Wenye malengo yao na kuwa na wavulana wasio na future, wale wavulana masharobaro, wanaotambia fedha za wazazi wao na kutembelea magari ya baba zao.
.
Mara wanapotambua muda umeenda ndipo hua desparate na Ndoa na hata wasiwe na clue yoyote.
.
Lakini nawaambieni, MUNGU wa Mbinguni hataacha Wanaume wanaomtegemea yeye wadharauliwe.
.
Mungu akam-replace Abigaili, mwanamke mwenye roho yake nzuri kuwa mke wa Daudi badala ya Mikali. Pia, Mungu Akam-replace Malikia Esta kuwa Mke wa Mfalme Ahusuero badala ya Vashti.
.
Pale utajapojiona wewe ni wa juu au unamdharau mwanaume uliye nae, MUNGU anaku-replace fasta!
.
Linapokuja suala la kuwa na life partner, Omba sana Hekima!
.
"Nao wakasema, “Basi, tumwite msichana mwenyewe, tumwulize, Wakamwita Rebeka na kumwuliza, Je, utakwenda na mtu huyu?” Naye akajibu,“Nitakwenda.” Mwanzo 24:57-58
.
Mungu akusaidie ewe Binti uwe na Hekima ili Ubavu wako asipate tabu kukupata....!!

By:
Tweve Hezron

Post a Comment

0 Comments