GIGY MONEY ANAKUPA UNACHOTAKA KWAKE, NI WEWE TUU

Ukimuona kwenye mitandao na ukikutana naye ‘live’ unaweza kukataa kuwa siyo mwenyewe. Ni msanii mwenye staili ya peke yake kwa namna alivyojiweka na kujitangaza mbele ya jamii.

Katika mitandao anaonekana pia ni msichana wa mjini, mwenye mambo mengi yasiyopendeza jamii.

Alianza kufahamika kama mpamba video za wasanii (video vixen), aliyepamba video za wasanii wengi katika muziki wa Bongo Fleva. Na picha zake tata alizokuwa akizitupia katika mitandao ya kijamii na alipokuwa akiulizwa na watu wa karibu au media kwa kutochagua maneno ya kuongea.

Huyu ni Gigy Money ambaye jina lake halisi anaitwa Gift Stanford ambaye anasema anakupa unachotaka. Gigy alianza kwa kusema watu wengi wanamuona hayupo sawa kiakili lakini yeye anajua nini anafanya kwani majibu anayoyatoa katika media huwa inategemea siku hiyo yuko katika ‘mood’ gani.

Anasema huwa anaangalia mazingira anayoulizwa maswali yako ya namna gani kama ya kupagawa basi na yeye anapagawa na kama ni ya utulivu basi na majibu yanakuwa ya utulivu.

“Unajua watu wanashindwa kunielewa mimi ni wa namna gani, wapo wanaoniona mimi kama chizi chizi tu na wapo wanaoniona kama sijielewi na maisha yangu, lakini wajue kuwa mimi nina akili timamu sema huwa nawafanyia kusudi media zinazokuja kuniuliza maswali ambayo hayana maana.

“Iko hivi, huwa najibu maswali kulingana na mazingira yaliyopo na hasa siku hiyo ukute nina ‘mood’ gani, kama nipo katika mazingira ya kupagawa na mimi nakupagawisha tu kama ya utulivu nakujibu kama hivi ninavyokujibu si unaona sina mapepe?”

Aidha Gigy anasema kwamba hapendezewi na baadhi ya watu wanaodhani anaigiza maisha kwani maisha anayoonekana kwa jamii ndio hayo hayo anayoishi.

“Mtu aliyebahatika kuniona maisha yangu ninayoishi ajue kabisa ndio hayo, mfano kuna kipindi nilipanga nyumba nikakwaruzana na mama mwenye nyumba kuhusu ulipaji kodi, yale ndio maisha yangu, sina maisha ya kitajiri ila tajiri ni roho yangu tu.”

Gigy anasema kwamba kuna utofauti mkubwa kipindi kabla hajawa msanii na sasa ni msanii, hivyo wale wote waliokuwa mastaa na kuwaona wako juu sasa anawachulia kawaida tu.

Post a Comment

0 Comments