DIAMOND PLATNUMZ AMCHOMESHA LEMUTUZ KWENYE PARTY

Le Mbebez! Downtown !Kura Maisha You Know!

Anga la burudani ndani ya Bongo na kule 254 siku ya jana na leo asubuhi zilisheheni manews ya kutosha juu ya kile kinachohapenika mitaa ya Mlimani City, Mastaa mbalimbali walitupie vyema na codes zao za black hivi, Kibembe kilikua kwa Lemutuz bana! Shuka tu uone

7/7 ilikua ni siku ya mfanano wa kuzaliwa kwa Mama wa Naseeb na pia kwa mchumba wake kutoka 254, Tanasha Dona. Ndani ya jiji la Dar es salaam sherehe hiyo ilipingwa bonge la promo kuanzia kwenye mitandao ya kijamii hadi kwenye tv, na bila kusahahu ilionyeshwa Live kupitia Wasafi Tv.

The Great Gatsby Eh!

Mastaa kibao walipita katika red carpet na huku wengi wakionyesha kuvaa mavazi nadhifu yaliyowapendeza wengi na Diamond Platnumz kuanikiza hilo kabla ya kuingia ukumbini alipost a pic ya Ricardo Momo na kuwaambia watu kuwa wale wanaokuja kwenye party sharti wapendeze bila hivyo wataaibika

Aliandika

Kama Haujapendeza Usipate tabu ya Kuja mana Utajiskia Vibaya…. #707TheGreatGatsby MLIMANI CITY NOW!!!


Bana si ndo Lemutuz akakatisha!

Watu mbalimbali walikua wanafuatilia tukio hilo LIVE  kupitia Wasafi Tv, walimuona mtu mzima William akikatiza na huku akiwa amevaa shati zake pendwa hivi, wananchi hapo hapo kwa wakareact kwenye post ile ile ya Mondy wakidai kuwa King huyo wa mitandao ya kijamii bongo kazingua codes.

Lemutuz alionekana kukaa meza moja na Jembe ni Jembe pamoja na mchekesheji Mpoki.

Angalia hapa reactions za wadau juu ya codes za Lemutuz:

Post a Comment

0 Comments