Huko wilayani Magu mkoani Mwanza kumeripotiwa kuwa kuna matukio ya wazazi kadhaa kutembea na watoto wao, suala ambalo ni kinyume na maadili na unyama uliopitiliza.
Kwa mujibu wa moja ya maafisa wa ustawi wa jamii wa wilaya hiyo, tayari mzazi mmoja ameshakamatwa na wengine wanafuatiliwa.
Amesema vile vile kuna sehemu maarufu kama Pango Hewa, ambapo wanafunzi hutumia kufanya vitendo vya ngono, suala ambalo ni kinyume cha sheria na utovu wa nidhamu na maadili.
Amesema mtoto yeyote awe mkubwa au mdogo atakayefanyiwa vitendo hivyo na mzazi wake au mtu mwingine yeyote basi lazima hatua za kisheria zichukuliwe.
Amesema tayari wameanza kupigia kelele matendo hayo ili kuwapa hali ya kujiamini watoto wote watakaokumbana na hali hiyo wasiwe na hofu kuripoti.
Amesema kuanzia mwezi Januari mpaka sasa, tayari kuna kesi mbili zimesharipotiwa ambapo kesi moja tayari imeshafanyiwa kazi.
0 Comments