ANERLISA AHARIBU MAHUSIANO YA BEN POL

Msanii wa bongo fleva ambaye alikua chini ya msanii Ben Paul, Wyse amefunguka ukaribu wake na msanii Ben Paul na kudai kuwa kwa sasa mahusiano yao sio kama zamani.

Ben Paul ndie aliyemtambulisha Wyse katika industry ya muziki wa bongo fleva kwa kufanya nae ngoma pamoja na kumsimamia kazi zake.

Kibao cha ‘bado kidogo’ ndicho kilichomtambulisha vyema katika anga la muziki nchini baada ya kushirikishwa na Ben Paul, ambae ndie aliyekuwa anasimamia kazi zake hapo awali.

Wyse kwa sasa ametoa kibao kinachokwenda kwa jina la ‘lini’ iliyorekodiwa katika studio za Free Nation ya Ney wa Mitego, kilichoshitua ni ukimya wa Ben Paul kutokupost ngoma hiyo ya kama alivyokua anafanya awali.

Kumekuwepo na hisia mbalimbali juu ya ukaribu wa Wyse na Ben Paul kupungua na huku wengi wakidai kuwa ni mahusiano yake na Anerlisa.

Akizungumza na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv  amedai kuwa ni kweli kwasasa mahusiano yake na mkali huyo wa RNB kuwa hawako karibu kivile kama zamani.

Ni kweli  Ben sasa hivi hatuko karibu sana unajua maisha yanabadilika…tunawasiliana kawaida siokama mwanzo na tulikua tunakaa wote ila kwasasa hatukai wote ilakitu kiko sawa alifunguka Wyse.

Na juu ya Anerlisa kuwa chanzo

Amefunguka

Inawezakana nayo ikawa facts watu wanahitaji privacy ..watu wanahitaji kufanya vitu vyao hauwezi kuwa hapo kila muda na huwezi kwenda kila wanapokwenda.

Wyse ameongeza kuwa bado mawasiliano yao yako vizuri na wanendelea kusuportiana.

Wiki iliyopita kumeripotiwa kuwa kulikua na sherehe ya kimila huko nchini Kenya na kusemekana kuwa Anerlisa na Ben Pol wamefunga ndoa ya kimila.

Hizi ni baadhi ya post za Anerlisa zinzobeba ushahidi juu ya hilo.

Hii pia

Post a Comment

0 Comments