Watu wengi hutamani kupata watoto mapacha,hii ni zaidi kwa upande wa wanawake. Kuna imani nyingi pia juu ya upatikanaji wa mapacha lakini kwanza kabisa ni muhimu kujua, nini hutokea hadi mtu anazaa watoto Mapacha?
Wataalamu wanasema, kinachotokea ni kwamba wanawake wenye asili ya mapacha kutoka kwenye vinasaba wanatoa mayai mawili kwa Kipindi kimoja.
Hivyo, kinachotokea, mayai yote yanarutubishwa na mbegu za mwanaume pindi wanapokutana kimwili na hii ni kesi ya mapacha wasiofanana.
Kwa wengine ambao huzaa mapacha wanaofanana, kinachotokea ni kwamba yai la mwanamke moja likishaungana na mbegu ya kiume linagawanyika mara mbili au tatu au hata nne na zaidi.
Hapo ndio watoto mapacha wenye kufanana wanatokea wawili, watatu na hata kuendelea. Wanafanana Kwasababu ni mbegu moja na yai moja linalotumika kwa watoto wote.
Kwa mwanaume inawezekana kusababisha mapacha endapo mwanaume mbegu yake moja iwe na viini viwili, hivyo ikiingia kwenye yai la mwanamke kila kiini kimoja mi mtoto mmoja na hivyo kutatokea watoto wawili. Ikitokea yai la mwanamke halija gawanyika baada ya kukutana na yai la Mwanaume lenye viini viwili watoto mapacha walio ungana watatokea.
Baada ya kujua utambulisho huo, ni njia zipi na vigezo gani vinaweza kumfanya mtu apate mapacha, Jarida kutoka ukurasa wa People’s lifestyle limeandika, soma hapa chini kujifunza:
Njia na Vigezo vya kupata watoto mapacha
kiukweli hakuna njia ya moja kwa moja ya kupata watoto mapacha lakini kuna baadhi ya sababu zinaongeza nafasi kubwa ya kubeba mimba ya watoto mapacha na tafiti nyingi zimeonyesha kwamba matumizi ya njia hizo yanaongeza nafasi kubwa sana ya kubeba watoto mapacha.
Chagua mpenzi wa aina hiyo
Kama unatoka familia ambayo mapacha wanazaliwa mara kwa mara uko kwenye uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha na kama ukizaa na mtu ambaye kwao kuna mapacha wa mara kwa mara basi na wewe una nafasi kubwa ya kuzaa mapacha. Kumbuka ni mwanamke tu, aliyetoka kwenye ukoo wa mapacha anaweza kuongeza nafasi ya kuzaa mapacha, mwanaume wa mapacha hawezi kuongeza nafasi ya kumpa mwanamke mimba ya mapacha.
Zaa umri ukiwa umeenda kidogo
Mwanamke akifkisha umri wa miaka 35 na kuendelea kunatokea mabadiliko ya mfumo wake wa uzazi kiasi kwamba mwili wake huanza kuachia mayai mawili kila mwezi badala ya yai moja kama ilivyokawaida, na hii huongeza nafasi kubwa sana ya yeye kubeba mimba ya watoto mapacha.
Matumizi ya dawa za uzazi
Kuna dawa ambazo hutumiwa na wanawake ambao wanashindwa kubeba mimba, dawa hizi hufanya yai zaidi ya moja kuachiwa kutoka kwenye mirija ya uzazi na hii huongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mapacha, na wanawake wanaotumia dawa hizi hujikuta wanabeba mapacha. mfano dawa za clomiphene citrate.
Kua na watoto tayari
Wanawake ambao wamezaa mtoto mmoja au wawili kabla wana nafasi kubwa sana ya kuzaa mapacha kuliko wale ambao hawajawahi kuzaa kabisa, ukifuatilia mapacha wengi hua hawazaliwi mimba ya kwanza ila kwanzia mimba ya pili kwenda mbele.
Kupata mimba ukiwa kwenye dawa za uzazi wa mpango
Japo sio rahisi sana lakini tafiti zinaonyesha kwamba mimba zinazoingia kwa bahati mbaya mwanamke akiwa anatumia dawa za uzazi wa mpango hutengeneza mapacha lakini pia mimba zinazoingia muda mfupi baada ya kuacha dawa za uzazi wa mpango hua zinaleta watoto mapacha.
Urefu na unene
Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake warefu wana nafasi kubwa sana ya kubeba mimba za mapacha kuliko wanawake wafupi, lakini pia wanawake wanaobeba mimba wakiwa wanene wanakua na nafasi kubwa sana ya kupata mapacha.
Vyakula
Jamii ambazo chakula chao kikuu ni viazi vikuu, zimeonyesha kua na mapacha wengi kuliko jamii zingine, tafiti zinasema kwamba viazi hivyo vina kiasi kikubwa sana cha homoni za oestrogen ambazo zinasababisha mama kutoa mayai mengi kitaalamu kama hyperovulation.
Kunyonyesha mtoto kwa muda mrefu
Kuna homoni moja inaitwa prolactin ambayo inahusika na kutoa maziwa kipindi mama ananyonyesha, kuendelea kuwepo kwa homoni hii kwa kiasi kikubwa wakati mama ameanza kushiriki tendo la ndoa kuna muongezea nafasi kubwa ya kupata mapacha akibeba mimba.
matumizi ya dawa za folic acid
Dawa za folic acid hutumika na wajawazito wote ili kuzuia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile hasa kwenye mishipa ya fahamu, lakini matumizi ya dawa hizi mwezi mmoja kabla ya kubeba mimba yanaongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mimba za mapacha.
kua pacha mwenyewe
Kama wewe mwenyewe ulizaliwa kama mapacha basi uwezekano wa kubeba mimba ya mapacha ni mkubwa sana kuliko wale wengine ambao walizaliwa kawaida
0 Comments