WANAWAKE WAZUIWA KUINGIA BAA, SOKONI USIKU...

UONGOZI wa Jimbo la Rutana katika eneo la Musongati umekataza wanawake kuingia katika baa au soko kuanzia saa 1:00 usiku bila kuambatana na mume wake.

Wanawake wamepinga hatua hiyo huku wanaume wakipongeza, kwa madai ya baadhi ya wanawake wamekuwa walevi na kushindwa kurudi nyumbani. Kiongozi wa eneo hilo, Jean-Damascene Arakaza, katika taarifa yake ameeleza kuwepo kwa baa katika mji wa Musongoti zinazochoma mbuzi na kunywa bia kukiwa na wanaume 30 na wanawake watatu wanaojadili maamuzi hayo.

“Ngoja ninywe bia yangu na kuondoka, huu ni unyanyasaji na ubaguzi kwa wanawake, kuna wanaume wengi wanakunywa na kurejea nyumbani wamechelewa kisha kuwapiga wake zao, je hawa hawahitaji kudhibitiwa,” alisema mmoja wa wanawake hao.

Katika eneo la Nyabitsindu, katika kituo cha Gisuriro, wanawake wameandamana kupinga maamuzi hayo, lakini baadhi yao wakikubaliana na maamuzi hayo. “Ni aibu kumuona mwanamke akitembea usiku,” alisema kiongozi wa wanawake katika eneo hilo.

Mwanaume kutoka jamii hiyo, Jean Ntamavukiro alimtakia maisha marefu kiongozi aliyetoa maamuzi hayo kwani kwa miaka kadhaa hajalala kitanda kimoja na mke wake kutokana na kushinda baa, hivyo uamuzi huo utaokoa ndoa yake.

Post a Comment

0 Comments