UWOYA ATAJA KOSA KUBWA ALILOWAHI KUFANYA KATIKA MAISHA YAKE

Muigizaji wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya, amefunguka kosa kubwa alilolifanya kwenye maisha yake na kusema kuwa kosa ni kumuamini kila itu anayemuona.

Uwoya amesema kuwa, huko nyuma alikuwa akimuamini kila mtu akijua ni watu wazuri kama alivyowachukulia na kuwaacha wawe karibu yake, jambo ambalo halikuwa sahihi.

“Hilo ndilo kosa kubwa ambalo nimelifanya katika maisha yangu kwa kuwaacha watu wakae karibu yangu kwa muda mrefu bila kujua wengine walikuwa ni nyoka,” alisema Uwoya.

(Visited 1 times, 1 visits today)

Post a Comment

0 Comments