USIOGOPE KUMWAMBIA MPENZI WAKO HAUJAFIKA KILELENI

Mambo muhimu ya kuzingatia unapokuwa faragha na mpenzi wako yaani namaanisha unapokuwa unajiandaa kufanya mapenzi.

Nadhani kila mmoja amenielewa namaanisha jambo gani. Hapa nataka tueleweshane jambo moja  la kuwa muwazi unapokuwa katika hilo eneo lako la kujidai.

Jambo la muhimu ni kumweka wazi mpenzi wako ili muende sawa katika ulingo wa mahaba.

Muambie mpenzi wako kuwa unahitaji kufika kileleni asikuachia njia panda hiyo ndio maana halisi ya tendo lenyewe.

Ukitaka kuufurahia mchezo huo kwa pamoja ni wote muwe mmefikishana kileleni.

Ninapozungumzia suala la kileleni ni mwanamke akojoe sio mwenza wako kila siku anakojoa wewe unabaki bila bila mnapofanya tendo la ndoa.

Ni wajibu wa mwanaume kukufukisha ingawa wapo wanaume ambao hujiangalia upande wake akishakojoa yeye basi hamjali mwenzake.

Mwanamke ni wajibu wako kumuambia mpenzi wako akufikishe pale mnapoanza mchezo usiogope kumuambia ukweli.

Wapo ambao wanazani kuwa ukimuambia ukweli mpenzi wako kuwa hajakufikisha atakuona kama wewe ni mhuni sio kweli.

Kwenye hiyo sekta kila mmoja ni mhuni kwa mwenzake ili kuupendezesha mchezo usikubali akuache bila kukufikisha kileleni.

Unapokuwa na mpenzi zaidi ya mwaka hajawahi kukufikisha kileleni jua anakukosea haki zako za msingi hili jambo la kufikishwa kileleni lina muhimu wake kwanza litakufanya ufurahi penzi lenyewe.

Mwanamke ili ufurahia tendo la ndoa ni kufikishwa kunakotakiwa kama una mwanaume hakufikishi jua unakosa vitu vitamu.

Ondoa uwoga kwa mpenzi wako na kabla hamjaanza muambie unahitaji akufikishe kileleni na kama mchezo umeisha wewe bado muambie hujanifikisha ili akianzisha game jingine akufikishe usione aibu kumueleza.

Unapokuwa muoga matokeo yake huwezi kufurahia penzi katika maisha yako huku ukiishia kusikia kwa wenzako jinsi wanavyofurahia.

Unapofanya mapenzi ni lazima mfurahi kwa pamoja usikubali kubaki nyuma katika eneo hilo ambalo ni muhimu kibinadamu.

Post a Comment

0 Comments