USIGOMBANE NA MWANAMKE MWENZAKO KISA MUMEO KACHEPUKA, FANYA HAYA


Kuna vitu muhimu ambavyo wana ndoa wanatakiwa kuzingatia hasa pale unapogundua mumeo ameanza ule mchezo wa kuchepuka.

Tumia muda mwingi kujiuliza ni wapi ulipokosea hadi mumeo kaanza kutoa penzi kwa mwingine.

Ukishafahamu makosa yako ni vizuri ukaanza kutengeneza penzi lako kwa mumeo ili aweze kumsahau mchepuko wake.

Baadhi ya vitu vidogo ambazo unavidharua kuvifanya kwa mumeo ama kuchukulia poa poa ndio vinavyomfanya atoke nje ya ndoa.

Kuna wanawake wanapogundua mume wake kachepuka basi hutumia nguvu kubwa kupambana na mchepuko na kujikuta unapoteza muda wako.

Katika hali kama hiyo utapambana na wangapi wengine hadi kupigana na mchepuko swali la kujiuliza utapigana hadi lini maana baada ya muda wanakutana na mumeo na mapenzi kuendelea.

Unapogundua jambo hilo huna haja ya kupambana na mchepuko rekebisha mapungufu yako utaona mabadiliko katika ndoa yako.

Unapoanza kugombana na mchepuko ni vigumu kuachana na mumeo utajikuta unapoteza muda wako pasipo na sababu za msingi.

Utagombana naye baada ya muda mfupi mumeo kaenda kumfuata tena wanabembelezana katika akili yako unajua wameachana.

Wapo baadhi ya wana ndoa kwa vile ameolewa wanajibweteka kwa madai yeye yupo ndani ya ndoa na kuanza kupunguza mapenzi kwa wanaume zao.

Ukipunguza  mapenzi kwa mumeo ni moja ya sababu ambazo zinasababisha mwanaume kutoka nje ya ndoa, hivyo usianze kupambana na mke mwenzako rekebisha ulipokosea.

Kama ulikuwa huandai chai anzaa sasa kumuandalia, ongea naye maneno matamutamu na kama hamna ratibu ya kutoka Out iweke muwe mnatoka hata mara moja moja.

Jitahidi kufanya majukumu yako kama mwanamke mfurahishe mumeo hasa unapokuwa kwenye sekta ya chumbani usijisahau kwa vile ameshakuoa usichukulie mazoea katika tendo la ndoa.

Post a Comment

0 Comments