SIRI YA WAPENDANAO KUISHI HADI KUZEEKA PAMOJA

KuWaKuta wapendanao wanaishi miaka nenda rudi kwa amani na furaha, si kazi ndogo. maisha ya uhusiano yana changamoto nyingi. mnaweza kuivuka hii, inakuja nyingine kali zaidi ambayo kimsingi mkizubaa tu inawasambaratisha. Ndiyo maana kizazi cha sasa tunashuhudia ndoa nyingi za vijana zikivunjika. Vijana wakishindwa kabisa kukabiliana na changamoto za uhusiano na kujikuta wameachana. Wanakosa uvumilivu na matokeo yake ndoa inayeyuka.

KWa nini YanatoKea? Ndugu zangu, haya yanatokea kwa sababu ya ujuaji. Kila mmoja anajifanya anajua mambo, yanatokea haya pia kwa sababu ya baadhi yetu kuwa jeuri. Kila mmoja anapokuwa jeuri kwa mwenzake, hapo ni tatizo, lazima kuwepo na maelewano. maeleWano YanaKuJaJe? Maelewano yanatengenezwa, kuna suala la uvumilivu. Ili muweze kuishi vizuri wapendanao wanatakiwa kuvumiliana. Mmekutana ukubwani kila mmoja akiwa na tabia zake, mnatengeneza umoja mpya hivyo kila mmoja anatakiwa kumvumilia mwenzake. Zibebe changamoto za mwenzako kama za kwako.

Kama kuna kitu anakukwaza na kweli unakiona kinakuletea shida, basi usikurupuke kutafuta suluhu. Tumia muda wako kuona namna ambavyo unaweza kumbadilisha arudi kwenye mstari. tumieni Busara Usitumie ubabe labda kwa sababu wewe ni mwanaume, tumia busara zaidi kumbadilisha mwenzako kutoka kwenye jambo ambalo wewe unaamini si zuri na unataka kumpeleka kwenyezuri. Ni tabia yake, aliijenga kwa muda mrefu, huwezi kuibadili kwa mara moja kama vile unazima swichi ya taa. msome viZuri mWenZi WaKo Waswahili wanakuambia siku huwa hazifanani, unatakiwa kulijua hilo.

Unatakiwa kumsoma mwenzi wako kwamba kuna kipindi anakuwa hayupo sawa. Usilazimishe kufikisha jambo lako siku hiyo maana kichwa hakiko sawa. Umjue mwenzako kwa undani kwamba anapovurugwa kazini au kwenye biashara zake anakuwaje. Badala ya kumuongezea matatizo, msaidie kwa kumliwaza. Usichochee moto wa ugomvi wakati mwenzako anapokuwa hayupo sawa. Una jambo lako, subiri wakati ambao utamuona mwenzako yupo kwenye ‘mudi’ nzuri. Marafiki zangu, kuna wakati mwenzi wako anaweza kuwa hajisikii tu kuzungumza.

Si kwamba anataka kukusaliti au kukufanyia jambo lolote baya, lakini hajisikii tu kuzungumza. tuJifunZe KuPitia WaZee Wetu Wazee wetu waliweza kudumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa na uvumilivu. Waliweza kubebeana changamoto zao. Kila mmoja aliweza kusimama kwenye nafasi yake. Mwanamke anajua wajibu wake kwa mumewe, vivyo hivyo mwanaume. Mwanamke haoneshi jeuri kwa mumewe,

mwanamke anamheshimu mumewe. Sasa hivi wanawake wanataka waheshimiwe kama si kusujudiwa na wanaume. Mwanamke anaendesha mashindano na mwanaume wake ili ikiwezekana ashike hatamu kwa ushindi wa jambo fulani. Kwa upande wa wanaume, wazee wetu walikuwa wanajua kuwapenda wake zao. Walikuwa wanawajali, wanawathamini kupita kiasi kwani walikuwa wanaelewa kwamba mwanamke si chombo cha kuteswa na kupigwa bali kuoneshwa mahaba. Wazee walielewa kwamba wanawake wanatakiwa kupewa zawadi kama vile vitenge na kadhalika. Mwanamke hata awe na kazi fulani yenye mshahara mkubwa, lakini hapati kiburi kwa mumewe. Anamheshimu kupita

maelezo. Hii ndiyo sifa ya wazee wetu kudumu kwenye ndoa. Hakuna changamoto iliyokuwa kubwa ya kuwafanya waachane. Wao walizibeba changamoto na kutafuta suluhu kwa busara na hekima hata kama kosa ni kubwa kiasi gani. tuJisaHiHisHe Turudi kwenye misingi mizuri ya wazee wetu. Utandawazi usitutoe ufahamu na kusahau misingi ya maisha ya uhusiano ya wazee wetu. Upendo wa kweli, kuheshimiana na kuvumilivu ilikuwa ndiyo silaha yao. Mkiyazingatia hayo, maisha mtayaona rahisi. unaweza kunifuata kwenye mitandao yangu ya kijamii, instagram&facebook natumia

Post a Comment

0 Comments