SHOGA MAARUFU WA NIGERIA AMWAGIA SIFA MUIGIZAJI TONTO DIKEH

Shoga maarufu kutoka Nigeria Bobrisky ameelezea jinsi anavyompenda mwigizaji nyota Tonto Dikeh na anaweza fanya lolote hata iwe kuuwa mtu ili awe kipenzi chake

Bobrisky amekuwa akimlimbikizia sifa chungu nzima mwigizaji huyo kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni na hata wawili hao wameonekana akiwa pamoja mara kadhaa.

Shoga maarufu wa Nigeria Bobrisky amlimbikizia sifa mwigizaji Tonto Dikeh

"Nakukosa sana, wewe ni kila kitu ninachohitaji maishani, wewe ni furaha yangu, mdundo wangu wa roho, nafsi yangu, pacha wangu, naweza nikauwa mtu ili niwe nawe," Bobrisky aliandika Instagram.

Bobrisky anajulikana kuwa shoga tajiri nchini Nigeria na pia mfanya biashara mkubwa hasa wa vipodozi na mapambo.

Post a Comment

0 Comments