MPENZI WANGU ANATAKA NIMPE MAPUMZIKO YA MIEZI MITATU, NIFANYEJE??


Mpenzi wangu wa miaka 3 anataka tupeana muda wa kupumzika wa miezi mitatu, anasema kwamba tunagombana sana na hakuna furaha tena kwenye mahusiano yetu na anahisi njia pekee ya kufanya au kurudisha mahusiano yawe mazuri ni pale tukipeana mapumziko ya muda wa miezi 3 ili kila mtu apate muda wa kujifikiria kama anamtaka mwenzie.

Katika hiyo miezi 3 hamna mtu anayeruhusiwa kufanya mapenzi na mtu mwingine. Mie tangia nianze mahusiano sijawahi kusikia watu kupeana mapumziko hata siku moja na mimi kama mwanaume rijali nitavumilia kweli muda wote huo bila kufanya ngono? sidhani!

Je, unadhani inaweza ikawa kwamba anataka kucheza cheza na wanaume wengine na ndo maana anataka muda wa kupumzika? simwelewi na wala sielewi haya mambo ya kupeana mapumziko. Niachane naye tu au nimvumilie?

Post a Comment

0 Comments