SIKU chache baada ya kutangaza kugeukia kwenye uigizaji, msanii wa Bongo Fleva, Meninah Atik ameamua kugeukia pia kwenye ushereheshaji wa maharusi ‘MC’ na kuwaambia wasanii wenzake kuwa wasipokubali kubadilika siku zote lazima watabaki hapohapo walipo kwa sababu sanaa inahitaji kubadilika.
Akizungumza na Za Motomoto, Meninah alisema kuwa nani alikuwa anajua kama anaweza kuwa MC mzuri na kila mmoja kumpenda kama tu asingeamua kubadilika, hivyo amewashauri wasanii wengine wabadilike pale wanapoona fursa.
“Msanii siku zote lazima uwe kama kinyonga, pale unapotakiwa kubadilika, fanya hivyo kwa sababu ukishikilia kitu kimoja unaweza kukosa fursa nyingine, mimi leo ni MC, lakini ningejiona keki si ningechina?” Alisema Meninah.
0 Comments