Wanaume wenzangu leo napenda kuwashirikisha namna ya kukwepa vizinga kwa mchumba, demu, mchepuko n.k.
Katika maisha yako epuka kujibu maswali yafuatavyo kutoka kwa michepuko;
1."Mambo mpenzi wangu" akakijibu "mabaya" usimuulize kwa nini? Atakujibu, "sina hela dear."
2."Maisha yanasemaje kipenzi changu?" Akakujibu, "maisha magumu hubby wangu ." Usimuulize kwanini? Atakujibu, "nimefulia mwenzio acha tu".
3. " Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho? Akakujibu, " sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi" usimuulize kwa nini?, atakujibu, "Yaani sina kitu mpenzi wangu, sina hata hela ya kubeep kwenye simu yangu."
4. Mwanamke akikuanza kwa gia hii, "nikuambie kitu kipenzi" wewe mkatalie kiutani utani kumbe moyoni uko serious. Hata akikomaa vip mbadirishie mada au mkaushie.
Hivyo utakuwa umekwepa kuingia kwenye mtego wa kupigwa kirungu jiepushe, mtoto wa kiume! Tokomeza virungu.
0 Comments