MANENO MATAMU YA "HAPPY BIRTHDAY" KWA KIM KARDASHIAN KUTOKA KWA KANYE WEST UTAYATAMI MWENYEWE

Maneno mataamu ya ‘birthday’ ya Kim Kardashian kwa Kanye West, utayatamani!!!

Jana ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa rapper kutoka nchini Marekani Kanye West ambapo mkewe kipenzi Kim Kardashian aliandika ujumbe mzuri kabisa kwenda kwa mmewe.

Kanye West na Kardashian ambao wamebarikiwa kupata watoto wanne mpaka sasa ni moja kati ya wanandoa maarufu ambao wanajishughulisha na tasnia ya muziki wenye amani na furaha kubwa kwenye ndoa yao.

“Happy Birthday. To my amazing husband, who never ceases to amaze me. Thank you for who you are, and all that you do. I love you!” ameandika Kim kupitia Twitter yake.

Akimaanisha “Furahia siku yako ya kuzaliwa. Kwako mme wangu wa pekee, ambaye huwa huachi kunishangaza. Asante kwa namna ulivyo nav yote unavyofanya. Nakupenda!”

Hivi karibuni wawili hao walibarikiwa kuongeza familia baada ya kupata mtoto wa kiume na kufanya idadi ya watoto kufika wanne.

Mtoto huyo ambaye wamempatia jina la Zaburi “Psalm”amepatikana kwa njia ya Mama mbadala (Surrogate Mother).

Post a Comment

0 Comments