KASHEHE: "Najifunza ku-date"

Na THOMAS MATIKO

KICHUNA mwigizaji nyota Brenda Wairimu kathibitisha kwamba uhusiano wake wa kimapenzi wa miaka minane na rapa Juliani umevunjika.

Mwaka 2018 alipoulizwa kuhusu maisha ya mahusiano yake na mwanamuziki huyo, Brenda alikiri kwamba walikuwa wakipitia kipindi kigumu.

Hata hivyo hivi majuzi alithibitisha kuachana huku akisema yupo singo na huenda ikamchukua muda kuingia katika mahusiano mengine.

“Sioni tatizo kuwa singo. Nilikuwa kwenye uhusiano kwa miaka minane kama sio zaidi. Kwa sasa najifunza upya kuwa kwenye mahusiano ila sina uhakika ni lini tena nitaingia kwenye uhusiano wa kudumu,” Brenda alisema.

Kwa kipindi chote hicho, mastaa hao wawili walijaliwa mtoto mmoja, binti Amor mwenye miaka mitatu kwa sasa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Juliani na Brenda kutemana kisha wakarudiana.

Iliwahi kutokea miaka ya nyuma kabla yao kujaliwa kumpata mtoto na waliporudiana ndipo Brenda akashika ujauzito.

Brenda pia aliwahi kukiri waziwazi kwamba ndiye alimtongoza Juliani.

Post a Comment

0 Comments