JINSI YA KUTUMIA MUDA VIZURI NA MWENZI WAKO BAADA YA KAZI

Mihangaiko ya maisha, inaweza kukufanya kuwa bize sana kiasi cha kukosa muda wa kukaa na mwenzi wako.

Unaweza jikuta kila siku una stresi za kazini, huna raha ya nyumbani, ukirudi wewe ni mtu wa kutaka upumzke tu, huna muda na mwenzio.

Badala ya kufanya mahusiano/ndoa yenu ikue, unajikuta unaharibu maana huna muda, sababu hamna maingiliano au mawasiliano mazuri.

Tena wengine husema, nikiwa nyumbani, bora nipumzike, nikiongea tu basi matatizo na ugomvi usio na msingi hutokea.

Kumbuka kwamba, muda unaoutumia na mwenzi wako ni mdogo sana ukitoa muda unaokuwa kazini na muda unaolala. Kwa nini uutumie muda huo kwa kugombana?

Unatumia muda mwingi kuinyenyekea kazi yako na kuipamba kwa sababu ndo inayofanya maisha yaende, vipi kuhusu mwenzi wako?

Kwa staili hiyo, utainjoi vipi maisha?

Ukweli ni kwamba, ni muhimu kutumia muda wako na mwenzi vizuri kabla hujaenda kazini, nahata unaporudi. Kabla hujaenda kazini unaweza ukaongea nae japo kidogo, mnaweza mkaongea maongezi yenu kama wandani.

Hakikisha vitu vya asubuhi kama nguo vimeandaliwa vizurisababu vitakuondolea wasi wasi na kwakua umeondoka mkiwa poa na mwenzi wako, basi siku inaweza enda vizuri.

Nini cha kufanya ili utumie muda vizuri na mwenzi wako?

Usianze mazungumzo na mwenzi wako mara tu unapoingia nyumbani, hii ni kwa sababu bado una uchovu wa kazini na pengine hata usafiri kurudi nyumbani.

Jipe muda wewe na mwenzi wako, mrelax kidogo, unaweza tumia muda huo kwa kuoga, uondoe uchovu, uwe msafi, unukie.

Ukisha pumzika/kurelax mchunguze kwanza mwenzi wako, je mudi yake na muonekano wake upoje. Kwa kua umemzoea, ni rahisi kujua kama hayupo sawa.

Kama hayupo sawa, baada ya muda kidogounaweza muuliza nini sababu ya yeye kuwa hivyo, kwa upole kabisa sio ukali. Mwambie maneno matamu, mfariji. Mwambie kwamba ana uwezo wa kuyavuka yote hayo kwani anaweza.

Baada ya hapo sasa waweza badili maongezi, ukaanza kumchekesha na mengine ya kufurahisha. Unaweza msimulia yaliyojiri ofisini na kumchekesha kuhusu mambo ya huko. Ukifanya hayo utaanza kujiona unarelax.

Kama mna watoto mnaweza mkawa nao, mkaongea, mkala pamoja au kufanya lolote la kufurahisha na kufanya usiku wenu uwe mzuri kama familia.

Nenda kitandani akili yako ikiwa imetulia/imerelax. Matatizo yanakuja na kuondoka, lakini muda unaotumia na mwenzi wako, hakika utawafanya kila siku mjione wapya. Maisha yenu na ndoa yenu yanahitaji sana ukaribu wenu.

Post a Comment

0 Comments