JINSI YA KUPUNGUZA KITAMBI KWA KUTUMIA LIMAO

Kama bado unatafuta njia rahisi na ya haraka kupunguza tumbo basi limao ni jibu lako.  Kutokana na kuwa na acid na vitamin C nyingi limao husaidia sana kupunguza uzito.

Limao husaidia mmeng’enyo wa chakula, hupunguza mafuta mwilini na hata kufyonza sukari mbaya.

Kutokana na hayo, limao laweza kukufanya upunguze mafuta tumboni bila hata kufanya mazoezi. Na kwa wale ambao matumbo yao huonekana makubwa sababu ya kutopata choo vizuri na kupelekea tumbo kujaa gesi, basi limao litakusaidia kupata choo vizuri na kuondoa gesi tumboni.

Je, ufanye nini ili upunguze tumbo kwa kutumia limao? soma namna nne za kutumia limao kwa matokeo mazuri:

Limao lililo changanywa na maji

Unaweza kuweka nusu kipande cha limao kwenye glasi au kikombe cha maji. Kwa matokeo mazuri, tumia maji ya uvuguvugu na kunywa mara mbili kwa siku. asubuhi kabla hujala kitu chochote, na jioni kabisa, masaa kadhaa baada ya kupata mlo wa usiku, hakikisha hauhisi shibe sana wakati unapokunywa maji hayo.

Wengine huweka malimao mawili mazima katika kontena lenye maji lita tatu, kasha hueka kwenye friji na kunywa mda wowote wanapojiskia kiu.

Angalizo ni kwamba, usipende kutumia limao kali wakati tumbo halina kitu, sababu hali hiyo itakuongezea aside tumboni.

Limao lililo changanywa na asali

Limao lililochanganywa na asali litapunguza mafuta ya tumboni kwa kasi. Asali ina virutubisho ambavyoo ni vizuri kwa miili ya aina zote na umri wowote na inapochanganywa na limao huleta matokeo chanya, na kama haupendi ladha ya limao peke yake basi asali ndo mkombozi wako.

Cha kufanya, changanya mililita 300 za maji ya uvuguvugu na kijiko kimoja cha chai cha limao na jijiko viwili vya asali kasha koroga na unywe.

Maganda ya limao

Kama ilivyo juisi ya limao, maganda ya limao tafiti zimegundua kuwa maganda ya limao yana ‘Pectin’ ambayo hupunguza ufyonzaji wa sukari mwilini. Hiii husaidia kuwa na uzito mzuri na kupungua kwa urahisi.

Cha kufanya, chemsha maganda kumi ya limao kwenye kiasi cha maji cha mililita 200. Acha maji yachemke kwa dakika 10, joto litasaidia kufyonza pectin iliyopo kwenye maganda ya limao. Yaache yapoe kasha kunywa, lakini aina hii itakua na ladha ya uchungu kiasi, hivyo unashauriwa kunywa  kabla ya kuswaki.

Unaweza kutumia limao kupunguza tumbo mpakapale utakapoona matokeo unayoyataka, haina muda maalum. Lakini tahadhari tu, limao hupunguza mwili pia.

Post a Comment

0 Comments