BOSTON, MAREKANI
SIKU chache baada ya kuachia albamu yake, Beauty Marks, nyota wa Pop duniani, Ciara Harris ‘Ciara’, amepata fursa ya kujiunga na masomo katika Chuo Kikuu cha Harvard, nchini Marekani.
Ciara, alisema muda mrefu alikuwa na shauku ya kusoma lakini anamshukuru Mungu tasnia ya muziki imemfikisha kwenye lengo hilo, kwani wiki hii amekubaliwa kujiunga na masomo.
Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili, atajiunga katika Chuo Kikuu cha Harvard kusoma masomo ya Biashara ya Muziki, Habari na Michezo chini ya Profesa Anita Elberse.
0 Comments