CARD B: MWILI NI WANGU NITAUTUMIA NINAVYOTAKA

LOS ANGELES, Marekani

WALE wanaodhani kumkosa Cardi B kwa kitendo chake cha kufanya upasauaji katika sehemu mbalimbali za mwili wake ni kumkomesha, basi imekula kwao.

Iko hivi, bibiye huyo amedai kuwa hatasita kufanya upasuaji endapo atahisi utamfanya aonekane vizuri kwani mwili ni wake na atautumia anavyotaka.

Msanii huyo alikumba na ukosolewaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wake kwa kitendo chake cha kufanya upasuaji baada ya kujifungua mtoto wa kike aitwaye Kulture.

Akiwajibu mitandaoni, Cardi alisema: “Nafanya upuuzi wowote ninaotaka kuufanya katika mwili wangu. Sina muda mchafu kama mlionao.”

Cardi B amekiri kuwa amepoteza mkwanja mrefu tangu madkatari walipomwambia apumzike kidogo kutokana upasuaji aliofanya.

Post a Comment

0 Comments