AMBER LULU AINGIA ANGA ZA SHILOLE

NA JESSCA NANGAWE
MSANII wa Bongofleva Lulu Auggen maarufu Amber Lulu amemtaka msanii mwenzake Shilole kupunguza mwili kwa madai utamkwamisha kufanya vyema stejini.

Umber Lulu amedai Shilole ambaye ni dada yake amekua akimshauri mengi na yeye akiwa mdogo wake anatamani kumuona na mwili wake wa zamani kwa kuwa ulikua unampa mwonekano mzuri zaidi ya sasa.
ìShilole ni dada yangu, amekua akinishauri hata kazi zangu za muziki, na mimi kama mdogo wake ikifika sehemu ya kumshauri natumia nafasi yangu, ni kweli kwa sasa ameongezeka mwili sana na natamani arudi kama awali kwani hapendeziîalisema Umber Lulu.

Msanii huyo kwa sasa ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ëMachozií ambayo inafanya vizuri akiwa kamshirikisha Marioo.

Post a Comment

0 Comments