
Huyu dada hapa mtaani kwetu huku Kwamtogole aliolewa na mume mchacharikaji mashallah, walijenga nyumba, mwanaume alianza biashara, alinunua dalala, nyumbani mboga si saba lakini mbili at tatu wana mudu.
Walibahatika kupata watoto wawili, wa kike na wakiume. Bi dada lakini hakua ameridhika na yule mwanaume. Yeye alimuona mshamba wala si wa level yake.
Siku ya siku yule baba wa watu amepata ajali. Alifariki, mirathi yote ameachiwa bi dada. Sasa ana raha yuko single na amempata kijana wa hadhi yake.
Yule kijana alianza kumwambia anampenda lakini hawezi kukaa kwenye nyumba ilyojengwa na mwanaume mwenzie. Hivyo waiuze waanze moja pamoja. Kweli cash waliyokua nayo walitafuta nyumba Sinza wakahamia. Nyumba aliyoacha marehemu ikauzwa.
Kijana ndiyo amekua father house. Kila kitu anasimamia yeye. Alianza kujenga, nyumba ilivyoisha alimleta mama yake kutoka kijijini. Dada ameanza kushinda na mama mkwe na kijana anamuambia mama yangu umhudumie.
Bibi ameanza commands ndani ya nyumba mpaka vitoto havina raha kwa kutumwa. Sasa dada ndiyo anaamka hataki tena ile hali. Anagundua kuwa nyumba na kiwanja hana jina lake.
Sasa ametafuta ndugu wa marehemu mume wake wamsaidie kupata mali zake.
Hivi unaweza kuwa na shamba la koroshao na ukaingia ubia na mtu mweye tuta la mchicha?
0 Comments