Kulizuka sokomoko ya aina yake Jumamosi, Aprili 27, katika kanisa la Mtakatifu James ACK Kiambu, baada ya jamaa aliyedaiwa kuwa mme wa mwanamke mwengine kufumaniwa akifunga ndoa na kipuza mwengine.
Mwanamme huyo ambaye taarifa kumhusu hazikubainishwa alisemekana kuwa alikuwa amewaajiri kwa muda walinda usalama ili kuwazuia wageni ambao walikuwa hawajaalikwa kuhudhuria sherehe hiyo.
Habari Nyingine: Diamond Platnumz amsajili baba yake katika lebo ya WCB ili naye ang’are kimuziki
Pete. Sherehe ya harusi yakumbwa na msukosuko baada ya mkewe halali wa bwana harusi kuzuru eneo la sherehe na kuzua rabsha Kiambu. Photo: Chicago Tribune. Source: UGC
Licha ya hayo, jamaa wa miraba minne ambao inaaminika walikuwa wakishirikiana na mke halali wa bwana harusi walivamia eneo hilo na kusambaratisha hafla hiyo.
Inaaminika kuwa, wawili hao walitengana awali na kesi ya talaka baina yao ingali mahakamani.
Hata hivyo, haijabainika iwapo sherehe hiyo ilisitishwa au la.
Mwaka wa 2018, wageni waliohudhuria harusi walilazimika kula chakula na keki iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo baada ya mke halisi wa bwana harusi na mwanawe kuvamia eneo la hafla na kuisambaratisha.
Elizabeth Wairimu aliyekuwa ameketi katika chumba ambacho chakula kilikuwa kinaandaliwa katika kanisa la St Mathews ACK alikuwa na ajenda moja- kuisitisha hafla hiyo.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.
0 Comments