JINSI YA KUGUNDUA TABIA YA MUME AU MKE WAKO

Ndugu yangu wala usipate tabu kugundua mkeo/mumeo ni kicheche/mpole/mkarimu/NK NK..unajua katika haya mahusiano kuna watu ni wasiri kiasi kwamba hata ungekua CIA au TISS usingeweza kugundua tabia zao maana hata hao walio kwenye hayo mashirika wake/waume zao wana wadanganya sana tuuuu.

Huna haja ya kila siku ukikutana nae/akirudi kutoka kazini kuchukua simu yake kukagua msg alizotumiwa na kutuma au simu alizopigiwa maana huko ni kujipa kazi na isiyo na malipo zaidi tu ya kujichosha.

NJIA PEKEE YA UHAKIKA NI HII

mkeo/mumeo/mchumba unapokutana nae Relax piga nae story then muulize MARAFIKI zake ni akina nani,yani jifanye unamwambia hivi baby ikitokea leo umesafiri halafu unataka kunipigia simu kujua naendeleaje ukakuta sipatikani Ni rafiki ako gani una muamini unadhani anaweza kuja kuangalia kama nipo salama au nina tatizo??

Lazima atakwambia na siku zote katika maongezi haya kua very romantic na mpole ili akwambie...akishakutajia Muulizetena BABY ebu nitajie TOP 10 yya marafiki zako unaowakubali/unaojifunza vitu kutoka kwao/unaowaamini ATAKWAMBIA.

Ukishawajua marafiki wa mume/mkeo Niamini leo nakwambia TAYARI UMESHAJUA TABIA YA MWENZA WAKO....kwa kua yeye kila kitu ni msiri anza kuchunguza tabia za hao marafiki alokutajia,ukikuta marafiki zake 10 wote ni wanaume macho juu juu basi kaa ukijua MUMEO nae ni macho juu akiwa huko nnje.

Ukikuta marafiki 8/10 wa mkeo ni wale wadada wa vigodoroni Kaa ukijua mkeo ana vichembe chembe vya hiyo TABIA,usimuhukumu kwa kua hujawahi mkuta ila tayari utakua unajua unaishi na mke/mume wa aina gani.

Kuna wanawake/wanaume kama mimi HATUNA MARAFIKI KABISA NDIO KUTUJUA TABIA ZETU YAKUPASA UTUMIE MODULA OBLONGATA IPASAVYO lasivyo ukitumia mbinu hiii hutofanikiwa kujua chochote.

Ukikuta mumeo/mkeo hana marafiki wa ajabu yupo yeye kama yeye au ukamuuliza marafiki zake akakwambia rafiki ake mkubwa ni MAMA AKE au kaka,dada ake au ndugu zake basi hao mimi huwa naonaga ndio wake/waume.

Usidanganywe na mtu eti marafiki zake wanatabia hizo ila yeye hana huo ni UONGOOOOOOOO mwanmke/mwanaume anaejielewa hawezi kuwa na rafiki mwenye tabia Mbaya alafu akabaki tu kuwa nae eti kisa ni rafiki ake...

MARAFIKI wa mwenza wako ndio TABIA YA MWENZAKO tia akilini hilo..ingia field uone kama sio kweli.

Post a Comment

0 Comments