Uwoya Amvaa Mwijaku Amtaka Kuacha Kufuatilia Maisha Yake


Jana Saa 2 Usiku Kupitia wasafi fm Star wa Filamu Irene Uwoya Alikuwa Kwenye Interview ya Kipindi cha Block89 na Moja Kati ya Swali aliloulizwa Kwenye Show ni Ukaribu wake na Mwijaku na Kwa nini Amekuwa Akimuongelea sana kwenye Mitandao ya Kijamii na Interview Tofauti.

Irene Uwoya Alisema kuwa Hajawahi Kukutana na Mwijaku na Wala Hana ukaribu nae, kwani hata anayoyaona Kwenye Mitandao ya Kijamii na Katika interview Tofauti Anayachukulia Kawaida na Kwake ni Kama Kichekesho tu

Leo Kwenye Ukurasa wake wa Instagram, Ameporomosha tena Onyo kwa Mwijaku na Kumuomba Aache Kufuatilia Maisha yake kwa sasa kwani hapendi Jinsi anavyoendelea Kumzungumzia

 "Hiii post ni ya saaa moja tuuu...nimekuangalia kwa mda mrefu sanaaa nimenyamaza ...kawaida sipendi maneno ila naona nikikaaa kimya unaniona zoba...ila niliamua kukaaa kimya sababu sibishanagi na wali mim...wewe mshenzi sindoulisababisha mpaka kipindi cha mahusiano kufa sababu ya umwali...staki kuongea sanaaa nakupa onyooo usije ukaniongelea tena kwenye maisha yako yote ...iwe mwanzo na mwisho"



Post a Comment

0 Comments