Kijana yeyote yule wa leo anatkiwa kujifunza mambo ambayo yatakuwa na mchango wa yeye kuweza kusonga mbele kwa namna moja ama nyingine. Yafutayo ndiyo mambo ambayo kijana wa leo anatakiwa kujifunza:
Epuka na ujitoe kabisa kutoka katika Kundi la watu wenye mitazamo hafifu juu ya maisha yao.
Acha kuwa king'ang'anizi kwa wale waliokutenga katika maisha yako.
Kuwa mtu wa haki na upendo hata kwa watu usiowajua.
Kuwa mtu wa heshima na upendo kwa kila mtu.
Kubali kuishi na watu kwa jinsi walivyo na sio wewe utakavyo.
Wahamasishe wenzio kufanya mambo yenye mafanikio na furahia mafanikio yao bila unafiki.
Kuwa mtu wa kuaminika kwa kila ukifanyacho
Samehe watu na endelea na maisha yako bila kuwafikiria tena
Kila siku fanya kitu kidogo kizuri kwa watu wakuzungukao
Kuwa makini na mwangalifu kwa hao unaowaita marafiki
Daima kuwa mkweli
Wasiliana na kuwa karibu na watu unaowajali katika maisha
Kuwa mtu wa kutimiza ahadi zako na kuwa mkweli
Toa kitu ambapo nawe unatarajia upokee
Sema unachomaanisha na maanisha unachosema
Uwe mtu wa kukubali na wengine watoe maamuzi
Ongea kidogo na kuwa makini katika kusikiliza
Usiwe mtu wa mabishano kila mara yasiyo na tija
Achana na umbea au maneno yanayoweza kuja kukunyima furaha
Uwe makini na mahusiano yako mwenyewe na mahusiano yako na MUNGU
0 Comments