Jambo muhimu unalopaswa kulifahamu kuhusu mafanikio ya maisha



Siku ya kadhaa zilizopita nilipata bahati ya kusoma kitabu fulani hivi kinachohusu mambo ya  mafanikio.

Mwandishi wa kitabu hicho ameandika mambo mengi sana kuhusu maisha kwa ujumla. Miongoni mwa mambo ambayo ameyaandika katika kitabu hicho ni pamoja na namna ambavyo watu wengi maisha yetu yanavyozidi kuwa duni kila jua lichomozapo.

Mwandishi wa kitabu hicho anasema ”watu wengi maisha yetu husasani katika suala la mafanikio yanakuwa duni kwa sababu ya tunashinwa kuishi vipaumbele vyetu binafsi katika maisha yetu”.

Suala la vipaumbele binafsi limekuwa ni tatizo kwa watu wengi, tatizo hili limewafanya watu wengi waendelee kulalamika ya kwamba maisha ni magumu sana kwa sababu ya kukosa msimo wa kuamini katika vipaumbele vyao.

Unapokosa msimamo wa kuendelea kusimamia kile unachokiamiani ndivyo hivyo unavyokosa  muelekeo wa kuteenda yale yaliyo ya msingi katika maisha yao ya kila siku.

Hii ni kwa sababu unaweza ukamkuta mtu fulani amepanga kufanya jambo fulani ila kwa sababu hii dunia ya watu wenye maneno watamshauri mtu huyo aachane na jambo hilo kwa kuwa halina manufaa, na kwa kuwa muhusika wa jambo hilo hana vipaumbele anavyoviamini atajikuta mwisho wa siku ameacha kufanya jambo hilo na kwenda kufanya jambo jingine.

Hivi hujawahi kukutana mtu amabye alipanga kujenga nyumba kama kipaumbele chake na kununua nyumba? Bila shaka umewahi kukutana na aina hii ya watu. Wengi wao ukiwachunguza utakuta wamebadilisha mawazo yao ya awali kwa sababu ya wamekutana na watu wengine ambao wameyabadili mawazo yao.
Kutokuishi kwa vipaumbele ni kubaya sana kwa sababu kunamfanya  mtu  husika kuyumbishwa sana katika maisha kwa yale anayoyaaona na kuyasikia.

Mtu akikuambia jambo fulani linafaa au lina faida sana  basi utajikuta unaacha kusimamia kile unachokiamini na kufanya jambo jingine ambalo mtu huyo amekushauri. Kwa tabia hii basi unatakiwa kusahau kuhusu mafanikio kwa sababu una ufinyu ndani mwako wa maamuzi ya kusimamia kile unachokiamini.

Mwisho naomba  niweke nukta kwa kusema yafutayo ”dunia hii imejaa maneno mengi sana, hivyo usipokuwa makini na maneno hayo utajikuta hakuna jambo la maana unalolifanya kwa sababu utakuwa ni mtu wa kuyumbishwa na kurudidhwa nyuma kimawazo na kivitendo kwa kutoka na watu wengine wanaokuzunguka.

Hivyo kila wakati unatakiwa kuelewa na  kujifunza kuishi kwa kuamini kile unachokiamini huku ukisimamia katika vipaumbele vyako,  acha  mara moja kuyumbishwa  na kuwa na tamaa na vipaumbele vya watu wengine kwa sababu kufanya hivi kutakutoa katika mstari wa mafanikio.

Maisha ni kuchagua, hivyo amua leo kuchagua kuishi na kuamini katika vipaumbele vyako.

Na: Afisa Mipango Benson Chonya

    

Post a Comment

0 Comments