Hiki ndicho alichoambiwa mama Ronaldo na mwanae



Mama mzazi wa nyota wa Juventus ya nchini Italia Cristiano Ronaldo, Dolores Aveiro ameeleza wazi alichoambiwa na mwanae baada ya kuondolewa kwa timu yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ajax ya nchini Uholanzi.

Ronaldo kwa kawaida amekuwa na sifa ya kutopenda kupoteza mchezo au chochote alichokuwa amedhamiria kukipata, kwa mujibu wa mama yake hiyo ndio hulka ya mtoto wake toka enzi zake za utoto lakini akipoteza mchezo anahisi upweke sana na kumweleza mama yake kwa upole na majonzi.
“Alikuja kwangu baada ya mechi kichwa chini, alikuwa mnyonge kwa sababu alikuwa akitaka kuendelea hadi fainali, aliniambia nimejaribu kadri ya uwezo wangu lakini siwezi kufanya miujiza. Mama samahani, maisha yaendelee” maneno ya mama yake Ronaldo akieleza mwanae alivyosikitishwa.

    

Post a Comment

0 Comments